Home »
siasa afrika
» SOMA SABABU ZILIZO PELEKEA MAHAKAMA INAYO SIMAMIA KESI YA RAIS MORSI YA MJINI CAIRO KUIAHIRISHA KESI HIYO
SOMA SABABU ZILIZO PELEKEA MAHAKAMA INAYO SIMAMIA KESI YA RAIS MORSI YA MJINI CAIRO KUIAHIRISHA KESI HIYO
Written By Unknown on Sunday, 16 February 2014 | Sunday, February 16, 2014
Mahakama moja mjini Cairo Misri
imeahirisha kesi ya aliyekuwa Rais Mohammed Morsi, baada ya mawakili
wake kuondoka mahakamani kwa hasira.
Mawakili hao wanalalamikia kile wanachosema ni
kuendelea kuzuiliwa kwa Morsi pamoja na waliokuwa wanachama wa vuguvugu
wa Muslim Brotherhood ndani ya chumba cha Glasi ambacho hakipitishi
sauti.
Duru zinasema kuwa mahakama itateua mawakili wengine kumtetea Morsi.
Kesi dhidi ya Morsi itasikilizwa tena Jumapili Ijayo
Mohammed Morsi akiwa mahakamani
Rais huyo wa zamani alipinduliwa na jeshi mwezi
Julai baada ya kutuhumiwa kwa kupanga njama na nchi za Magharibi ,
utawala wa Pallestina Hamas, kundi la Hezbollah nchini Lebanon na
serikali ya Iran kupanga mashambulizi nchini Iran. Hii ni moja ya kesi nne zinazomkabili Morsi pamoja na maafisa wakuu wa Muslim Brotherhood.
Iwapo atapatikana na hatia bwana Morsi anakabiliwa na hukumu ya kifo
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!