Subiri, huna haja ya kuumiza kichwa. Supastaa wa
Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Coast, Yaya Toure, amepenya
kwenye Kumi Bora ya wanasoka wenye thamani kubwa zaidi duniani kutokana
na staa huyo kuingiza Dola 20 milioni kwa mwaka tangu alipotoka
Barcelona na kuhamia England.
Hata hivyo, makala haya yanakuletea wanasoka
watano bora wenye thamani kubwa zaidi duniani ambao bado wanatamba
kwenye soka kwa sasa.
Kiungo fundi wa Barcelona na Hispania, Andres
Iniesta anashinda kila kitu kwenye maisha yake ya soka. Jambo hilo na
ubora wake wa ndani ya uwanja umempandisha thamani na kutajwa kuwa na
thamani ya Dola 78 milioni.
Katika kuthibitisha thamani ya mchezaji huyo kuwa
ni kubwa, klabu ya Barcelona imeweka kipengele cha kulipwa Dola 206
milioni kwenye mkataba wake kama kutakuwa na timu inahitaji huduma ya
staa huyo.
Thamani Dola 82 milioni
Klabu ya AS Monaco ya Ufaransa ililazimika kutumia
pesa nyingi kuhakikisha inarudi kwa kasi na kuwa tishio kwenye Ligi Kuu
Ufaransa.
Katika kulifanya hilo, Monaco ilizama mfukoni na
kumnasa staa wa Colombia, Radamel Falcao, kutoka Atletico Madrid na
kumpa mkataba wenye thamani ya Dola 82 milioni. Kwa sasa staa huyo ni
majeruhi, lakini alifunga mabao tisa kwenye mechi 13 kuthibitisha
thamani yake.
3. Lionel Messi
2. Gareth Bale
3. Lionel Messi
Tuzo nne za Ballon d’Or kibindoni, jambo hilo
limemfanya staa huyo wa Argentina kuweka kibindoni Dola 118 milioni.
Wakati huo huo klabu ya Barcelona ipo kwenye mchakato wa kumpatia
mkataba mpya mchezaji huyo ambao utakuwa mnono zaidi huku kwenye mkataba
wake kumewekwa kipengele kinachohitaji ilipwe Dola 797 milioni kama
kutakuwa na timu inataka kumsajili.
2. Gareth Bale
Kuondoka Tottenham Hotspur ni kitu kilichofanya
tofauti kubwa katika maisha ya staa huyo wa kimataifa wa Wales kutokana
na jambo hilo kumletea pesa nyingi. Winga huyo wa zamani wa Southampton
ametua Real Madrid na kupewa mkataba wenye thamani ya Dola 138 milioni
kwa maana ya kupokea Dola 487,000 kwa wiki.
Mara kadhaa amekuwa akihusishwa kwenye michezo ya kompyuta na kulifanya jina lake kuwa nembo kubwa katika wigo wa biashara.
Thamani Dola 150 milioni
Cristiano Ronaldo kwanza ni mwanasoka wa kwanza
kufikisha wafuasi 50 milioni kwenye ukurasa wake wa Facebook. Lakini,
kwenye kiwango cha pesa, staa huyo wa Real Madrid na Ureno anaripotiwa
kuwa na kipato kinachofikia Dola 150 milioni. Ronaldo Januari mwaka huu
alitwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Fifa kitendo ambacho
kimemwongezea thamani zaidi.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!