Sir Alex Ferguson amefunguka kwamba alimwambia mkurugenzi mkuu wa Manchester UNITED David Gill kuweka bei ya £150 million kwa timu yoyote ambayo ingetaka kumsajili Cristiano Ronaldo.
Ronaldo
alijiunga na miamba ya soka ya Spain mnamo mwaka 2009 kwa ada ya
uhamisho iliyoweka rekodi ya dunia £80million lakini Ferguson anaamini
Raisi wa Real Madrid Florentino Perez angeweza kulipa mara mbili zaidi
ya fedha ya hizo walizolipa kumpeleka mwanasoka bora wa dunia Santiago
Bernabeu.
Katika
mahojiano na gazeti la AS, Ferguson alisema: "Nilimwambia David Gill
apange bei ya £150 million. Perez angeweza kulipa hicho kiasi cha
fedha."
Lakini
matakwa ya kocha huyo hayakusikilizwa na Gill. "Kitu pekee
kinachoniumiza nililisema hili kwa David Gill mara nyingi, kiasi ambacho
amekitaja kwa Real hakikuwa sahihi.
"Nilimwambia David, taja kiasi cha £150m.' 'Acha ujinga," akaniambia. 'Hawawezi kulipa kiasi hicho."
Lakini,
Real walivunja rekodi ya usajili kwa kutumia kiasi cha £85 million kwa
ajili ya kumsajili winga wa Wales Gareth Bale, jambo lilopelekea
Ferguson, 'Vipi kama tungewaambia walipe £150m???"
"Najiuliza
kila siku Perez angesema nini kama tungewaabia walipe £150m.
Ukizingatia wamemsajili Gareth Bale kwa £85 million, naamini wangekubali
kulipa kiasi cha zaidi ya £80m .
"Nina uhakika, kwa sababu
Perez alikuwa anajua kabisa aina ya ubora mchezaji aliokuwa nao, kama
takwimu za Cristiano zinavyoonesha."
Winga
huyo mreno, ambaye alijiunga na United kutoka Sporting Lisbon 2003,
tangu wakati huo mpaka leo ameshafunga mabao 238 katika mechi 233 akiwa
na Real Madrid pia alifunga mabao 91 katika misimu yake mitatu ya mwisho
Old Trafford.
"Kama
tungelipwa £150 million, ningeongea kuhusu hilo jambo kwa kipindi chote
kilichobaki cha maisha yangu, kwa sababu ingekuwa jambo kubwa na zuri
kupokea kiasi hicho cha fedha, sio tu kutoka kwa Madrid bali timu
yoyote.
"Hata hivyo, Cristiano aliondoka akiwa na baraka zangu na tulipata kiasi kikubwa cha fedha."
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!