Rapper wa Nidanganye, Shetta aka Baba Qayllah ambaye ni mwana-ndoa tangu miaka miwili iliyopita amezungumzia maisha yake ya ndoa yanavyomsaidia katika kazi yake ya muziki.
Tofauti na baadhi ya wasanii wengi vijana ambao hudai kuwa ukiwa katika ndoa baadhi ya mambo ya career yako yanakuwa katika wakati mgumu au hata kuharibika kabisa, Shetta anaona maisha yanaenda kwenye mstari ulionyooka.
“Hii ni part ya kimaisha, sio time yako imefika kwa sababu ya muziki unaogopa eti usioe, no, mimi kwangu hiyo haipo. Muziki wangu uko pale pale, show napiga palepale, yaani nikiingia kwenye show ni mashangwe yaleyale. Kerewa ipo, Sina Imani ilipita, Nidanganye… nilioa tangu Nidanganye huko na vitu kama hivyo. Unaona muziki wangu unaendelea.” Shetta ameviambia vyombo vya habari.
“Cha msingi na cha secondary ni kwamba wasiogope, watu wengi wanaogopa kwa sababu ya ile mchepuo chepuo njia za nje.” Ameongeza kuwa yeye anaenjoy maisha ya ndoa kiasi kwamba yanamsaidia kiuchumi pia kuhifadhi anachopata kwenye muziki.
“Mimi naenjoy zaidi, na nafikiri inanisaidia kuhifadhi pesa zangu, yaani unajua kuna uoga fulani wa kimaisha tofauti na unapokuwa single tu kwamba ‘aah babu eeh pesa zipo ntatumia’. Lakini unapokuwa na familia unajua imepatikana pesa unakuwa unawekeza unafanya hichi na hichi nini, hivyo yani.” Amesema Baba Qayllah..
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!