Winga wa klabu ya Bayern
Munich amebainisha kuwa alitumia siku ya mazoezi ya Jumatano kufanya
kazi ya kupiga mipira ya krosi kwa mguu wake wa kulia ambao hautumiagi
na juhudi hizo zimezaa matunda kwa kuivusha timu yake hatua ya nusu
fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Mabingwa hao
watetezi walifungwa bao la kuongoza na Manchester United katika Uwanja
wa Allianz Arena kwa shuti kali la Patrice Evra lakini Mario Mandzkuic
aliharibu sherehe hiyo kwa kusawazisha dakika chache baadae. Robben
alimpigia krosi kwa mguu wake kulia Thomas Muller aliyefunga bao la pili
kabla ya yeye kufunga la tatu na kuifanya Bayern kuibuka na ushindi wa
mabao 3-1 katika mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa. Akihojiwa mara
baada ya mchezo huo Robben amesema mara baada ya kumaliza mazoezi ya
asubuhi jana alikuwa akitaniana na wenzake na kujaribu kupiga krosi kwa
kutumia mguu wake wa kulia jambo ambalo limemsaidia. Bayern wataingia
katika upangaji wa ratiba ya nusu fainali Ijumaa sambamba na Atletico
Madrid, Real Madrid na Chelsea ambazo naqzo zimevuka hatua hiyo.
Home »
michezo ulaya
» HABARI ZASEMA KUWA KABLA YA MATCH YA MAN-UTD NA B.MUNICH ROBBEN ALIFANYA MAZOEZI NA MGUU WAKE WA KULIA
HABARI ZASEMA KUWA KABLA YA MATCH YA MAN-UTD NA B.MUNICH ROBBEN ALIFANYA MAZOEZI NA MGUU WAKE WA KULIA
Written By Unknown on Thursday, 10 April 2014 | Thursday, April 10, 2014
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!