PEP
Guardiola ameeleza kuwa kiwango walichoonesha Bayern Munich ni kikubwa mno
japokuwa walifungwa mabao 4-0 na Real Madrid katika mchezo wa nusu fainali ya
pili ya UEFA kwenye uwanja wa Allianz Arena jana.
The
Bavarians walichanganyikiwa kwa mabao mawili ya Sergo Ramosi na Cristiano
Ronaldo na kuvuliwa ubingwa kwa wastani wa mabao 5-0 kufuatia kupigwa bao 1-0
mchezo wa kwanza Santiago Bernabeu.
Guardiola
ambaye kikosi chake kilicheza kwa kujituma zaidi katika kipigo cha kwanza cha
bao 1-0 Bernabeu, hakikuweza kufua dafu jana Allianz Arena.
“Kila
kitu kinatokea katika mpira kutokana na kucheza vizuri. Nimefungwa mara nyingi
katika kazi yangu na hii ni mojawapo”. Guardiola amewaambia waandishi wa
habari.
“Tulifungwa
mabao mengi, lakini tulicheza kwa kiwango kikubwa na ndio sababu ya kupoteza”.
“Hakuna
sababu nyingine, huu ndio mpira”.
“Unapocheza
vibaya, unafungwa mabao mengi. Tuliingia na nguvu, tungeweza kufunga kwa nafasi
tulizopata, lakini hatukuweza”.
“ Kucheza
kwetu vibaya ndio sababu pekee ya kufungwa”.
Bayern
imefanikiwa kutwaa kombe la dunia la klabu na Bundesliga msimu huu, na
wamebakiwa na kombe la mwisho la DFB-Pokal mei 17 dhidi ya Borussia Dortmund.
Hii
itakuwa kama marudio ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka jana.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!