Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » LEO KATIKA HISTORIA

LEO KATIKA HISTORIA

Written By Unknown on Friday, 25 April 2014 | Friday, April 25, 2014

Ordibeheshti mwaka 1359 Hijiria Shamsia, Marekani ilishambulia kijeshi ardhi ya Iran kwa kutumia helikopta na ndege kadhaa za kivita. Serikali ya Marekani ilifanya mashambulizi hayo baada ya kushindwa njama zake mbalimbali za kutaka kuuangusha utawala wa Jamhuri ya Kiislamu wa Iran. Hata hivyo mashambulizi hayo yalikatishwa na tufani kubwa ya mchanga iliyopelekea kuanguka baadhi ya ndege, kushika moto helikopta za Marekani na kuuawa baadhi ya askari wa nchi hiyo huku waliobakia wakiikimbia ardhi ya Iran.

     ************************************************************
 
Siku kama ya leo miaka 43 iliyopita Wamarekani laki mbili walifanya maandamano mjini Washington wakiendeleza upinzani wao dhidi ya mashambulizi ya nchi hiyo huko Vietnam. Maandamano hayo yalikuwa miongoni mwa vielelezo vikubwa vya upinzani wa wananchi wa Marekani dhidi ya siasa za kichokozi za serikali ya nchi hiyo huko Vietnam. Katika vita vya Vietnam vilivyoanza mwaka 1964 Marekani ilituma askari laki tano nchini humo ambako makumi ya maelfu miongoni mwao waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Kwa sababu hiyo wananchi wa Marekani walizidisha upinzani dhidi ya vita hivyo na mwaka 1975 Marekani ililazimika kufunga virago na kuondoka Vietnam kutokana na mashinikizo ya ndani na ya kimataifa na kushindwa mara kwa mara jeshi la nchi hiyo katika medani za vita.

    ************************************************************

Na siku kama hii ya leo miaka 726 iliyopita yaani mwezi Jamadithani mwaka 709 Hijria alifariki dunia mtaalamu wa hadithi, mfasiri wa Qur'ani, faqihi na mtaalamu wa lugha wa zama hizo Ibn Ataaullah aliyekuwa mashuhuri kwa lakabu ya Sheikh Kabiib. Alizaliwa Cairo huko Misri katika familia ya kidini na kupata elimu na maarifa ya kidini katika mji huo. Mwanazuoni huyo mkubwa wa fiqhi alikuwa akiamini kwamba miongoni mwa nyadhifa za maulamaa ni kuwanasihi na kuwaongoza viongozi na masultani.
Miongoni mwa vitabu vya mwanazuoni huyo ni Al Hikamul Ataiyya na Al Munajatul Ataiyya.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi