Mchambuzi mahiri wa soka nchini,Uingereza,Alan
Smith anahisi kuwa kupangiwa na Atletico Madrid itakuwa matokeo mazuri
zaidi kwa Chelsea katika droo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya Ijumaa.
Kikosi cha Jose Mourinho kilifanikiwa kuitoa
Paris Saint-Germain kwa goli la ugenini siku ya Jumanne usiku na kipo
katika changamoto kubwa ya kushinda michuano hiyo huku kukisubiriwa droo
ya nusu fainali itakayofanyika Nyon.
Smith anaamini kuwa ubora wa safu ya ulinzi ya
Chelsea unawapa nafasi ya kuweza kulitwaa taji hilo jijini Lisbon mwezi
Mei 24 lakini anaamini kuwa Bayern Munich na Real Madrid wapo katika
nafasi nzuri zaidi ya kutwaa taji hilo.
Huku akisema kuwa,Mourinho huenda akawa na
furaha zaidi iwapo atakutana na vinara wa ligi kuu ya Uhispania,Atletico
kwenye hatua hiyo ya nne bora.
Na alipoulizwa kuwa timu ipi Chelsea wanataka
kuikwepa,mchambuzi huyo alisema kuwa”Bayern namba moja halafu wanafuatia
Real Madrid unaweza kupata picha hapo.”
“Hatuwezi kufikiri Chelsea wamekuwa na ubora
wa kutosha kwa miaka kadhaa iliyopita na walimaliza kwa kushinda
hili.Bado wamepata safu ya ulinzi imara zaidi na sasa wapo vizuri zaidi
kwa hilo.”
Smith akaongeza kuwa,”Unaenda kwa njia ndefu
kuifunga beki ya kati iliyokuwa na ushirikiano bora wa John Terry na
Gary Cahill pamoja na Ivanovic,Azpilicueta na kipa mzuri sana pia yote
hayo chini ya meneja mwenye mbinu kali.
“Kama wanazuia kwa jinsi walivyo wanaweza kuwa
wagumu zaidi na walichokipata kutoka kwa PSG usiku ule wanapaswa kuanza
kuamini jina lao limeandikwa tena kwenye Kombe.”
Lakini akasema Real Madrid dhidi ya Bayern
Munich itakuwa kama fainali na anafikiri kuwa kuna timu mbili bora zaidi
katika michuano hiyo na utapenda kutaka kuziona timu hizo mbili
zikipambana pamoja.
Pia akasisitiza kuwa timu ya Diego Simeone
nayo inanafasi nzuri ya kushinda ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa mara
ya kwanza na kudai ushindi walioupata dhidi ya Barcelona siku ya
Jumatano haukuwa rahisi hata kidogo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!