Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , , , » BAADA YA MKE WA RAIS WA MAREKANI KUTUMA UJUMBE KWA BOKO HARAM WATU WENGINE MASHUHURI WAENDELEA NA WAO KUAGIZA UJUMBE KWA KUNDI HILO

BAADA YA MKE WA RAIS WA MAREKANI KUTUMA UJUMBE KWA BOKO HARAM WATU WENGINE MASHUHURI WAENDELEA NA WAO KUAGIZA UJUMBE KWA KUNDI HILO

Written By Unknown on Friday, 9 May 2014 | Friday, May 09, 2014

Kikundi cha kigaidi cha Boko Haram cha Nigeria kimeendelea kuwashikilia wasichana 200 wa shule waliotekwa nyara na kikundi hicho katika kipindi cha wiki tatu zilizopita huku raia wa Nigeria wakifanya maandamano kushinikiza serikali kuongeza juhudi za kuwatafuta na kuwaokoa wasichana hao.
Raia hao wa Nigeria wameanzisha kampeni iliyopewa jina la la Warudisheni Wasichana Wetu ‘Bring Back our Girls’ na imeungwa mkono na serikali za nchi nyingi kubwa duniani ikiwa ni pamoja na China Canada, Uingereza na Marekani huku rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan akiahidi kuwa serikali yake itawasaka popote walipo na itawaokoa.

Watu mbalimbali maarufu duniani wameungana na kampeni hiyo katika mitandao ya kijamii na kupost picha wakiwa na mabango yaliyoandikwa ‘Bring Back Our Girs’.
Malkia wa talk Show Oprah Winfrey, Michelle Obama, Kim Kardashian, Puff Daddy na John Legend pia ni miongoni mwa watu hao, huku Tanzania pia ikiwakilishwa na watu mbalimbali.

Puff Daddy yeye ameongeza msisitizo kwenye bango lake kwa kuandika “Bring Back Our Girls ‘Now”. Bango la John Legend yeye amewatupia dongo Boko Haram waliodai kuwa watawauza wasichana hao, “Real Men Don’t Buy Girls..”
Polisi nchini Nigeria wametangaza donge nono kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia upatikanaji wa wasichana hao.
Kundi la Boko Haram limedai kuwa linawashikilia wasichana hao kama sehemu ya kampeni yao ya kupinga elimu ya magharibi na linawataka wasichana wanafikisha umri wa utu uzima waolewe na waachane na kile wanachokiita elimu ya magharibi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi