Baada ya kuhesabiwa baadhi ya kura
za uchaguzi mkuu nchini Afrika Kusini, chama tawala cha African National
Congress (ANC) kinaongoza katika uchaguzi huo. Tume ya uchaguzi ya
nchi hiyo imetangaza kuwa, baada ya kuhesabiwa asilimia 31 ya kura, ANC
imepata asilimia 58.7 ikifuatiwa na chama cha Muungano wa Kidemokrasia
kilichopata asilimia 27.7 ya kura huku chama cha Wapigania Uhuru wa
Uchumi kikipata asilimia 4.2.
Tume ya uchaguzi ya Afrika Kusini
imetangaza kuwa, uchaguzi huo mkuu wa jana ulifanyika kwa amani katika
maeneo yote na kwamba wananchi walijitokeza kwa asilimia 72 kupiga
kura. Iwapo chama cha ANC kitashinda kitamuwezesha Rais Jacob Zuma
kuendelea kuiongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa pili wa miaka
mitano.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!