Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HABARI KUTOKA UGANDA ZASEMA KUWA WAKIMBIKIZI WENYE ASILI YA CONGO WALIYOMO NCHINI HUMO WAPANGWA KUREJESHWA MA KWAO

HABARI KUTOKA UGANDA ZASEMA KUWA WAKIMBIKIZI WENYE ASILI YA CONGO WALIYOMO NCHINI HUMO WAPANGWA KUREJESHWA MA KWAO

Written By Unknown on Monday, 5 May 2014 | Monday, May 05, 2014

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewatolea mwito raia wake wanaoishi Uganda kama wakimbizi waanze kujiandaa kurudi nyumbani kwa sababu usalama umerejea nchini mwao. Wito huu ulitolewa baada ya kumalizika kwa mkutano wa siku tatu siku ya Jumatano terehe 30 April, uliokuwa unafanyika mjini Kampala kujadili njia za kuwarudisha wakimbizi nyumbani mwao.
Maafisa kutoka serikali ya Congo, Uganda na Idara ya Umoja wa Mataifa inayoyashughulikia maslahi ya wakimbizi UNHCR waliamua kukutana na kujadili njia salama za kuwarudisha wakimbizi Wakongomani nyumbani baada ya boti lililokuwa linawabeba wakimbizi waliokuwa wametoroka kwenye kambi ya wakimbizi ya Kyangwali nchini Uganda kuzama wakiwa safarini kurudi nchini Congo mwezi uliopita. 
Sasa, wakimbizi ambao wanataka kurudi nyumbani kuanzia leo wako huru kuomba msaada kutoka UNHCR warudishwe nyumbani lakini zoezi la kuwarudisha nyumbani litazinduliwa rasmi mwezi wa tisa mwaka huu.
Waziri wa usalama wsa ndani wa DRC, Richard Mangezi, amesema "Serikali za Congo na Uganda pamoja na UNHCR , zitatayarisha mpango wa kuweza kuwarudisha wakimibizi wote nyumbani. wakti huo huo jeshi letu la Congo na wanajeshi wa MONUC wanafanya jitihadi kumaliza hali ya uwasi na ninadhani katika muda wa siku 45 mambo yatakuwa yamekamilika."
Baadhi ya wakongomani niliozungumza nao wanasema hawako tayari kurudi nyumbani.
Serikali ya Uganda imepewa jukumu la kuhakikisha kwamba kabla ya mwisho wa mwezi wa saba, inafanya utafiti ili kujua kama wakimbizi Wakongomani  wanauelewa mchakato huu wa kuwarudisha nyumbani na pia kujua idadi kamili ya wakongomani wanaotaka kurudi nyumbani.

Wakongomani pia watahamasisha kuhusu zoezi hili. Serikali ya Uganda imekaribisha zoezi hili la kuwarudisha Wakongomani nchini mwao. Mapema mwaka huu, Uganda ilianzisha kampeni ya kuchangisha dola milioni 86  za Kimarekani ikisema haikuwa na uwezo tena wa kuwahudumia wakimbizi wote.

Nchini Uganda kuna wakimbizi  elfu mia tatu sabini  na nne. Congo ndio inayoongoza ikiwa na wakimbizi elfu mia moja themanini na nne. Inafuatwa na  Sudan kusini ikiwa na wakimbizi elsfu tisini na tatu. Somalia nayo inashikilia nafasi ya tatu ikiwa na wakimbizi  elfu arobaini na moja. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa wizara ya majanga na wakimbizi.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi