Hatimaye Jay Z, Beyonce na mdogo wake Solange wametoa tamko rasmi
kuhusu ugomvi uliotokea kwenye lift na video yake kusambaa kwenye
mitandao ikimuonesha Solange akimpiga makofi na mateke Jay Z.
Watatu hao waliandika tamko lao na kulituma kwa Associated Press, May 15.
Wanafamilia hao kwa pamoja wameeleza katika tamko lao kuwa wameyamaliza matatizo yote kama wanafamilia na kwamba ni kawaida kwa familia zote kugombana na wao ni sehemu ya familia hizo pia.
“Kutokana na press release iliyotolewa ya video ya tukio lilitokea kwenye lift kuanzia Jumatatu, May 5, kumekuwa na usambaaji mkubwa wa maelezo kuhusu nini kilisababisha tukio hilo. Lakini kitu cha muhimu zaidi ni kwamba familia yetu imeshalishughulikia na limeisha.
“Jay na Solange kila mmoja amechukua jukumu lake kwa kile kichotokea. Wote wametambua nafasi yao waliyohusika katika hili suala la faragha ambalo limetolewa hadharani. Wote wameombana msamaha na tunaendelea mbele kama familia iliyoungana.” Wameandika katika tamko hilo.
Hata hivyo wamekanusha ripoti zilizoeleza kuwa katika siku hiyo Solange na alikuwa amelewa sana na kwamba muda wote alikuwa akionesha tabia sizizo za heshima.
“Mwisho wa siku familia zote zina matatizo na sisi hatuko tofauti. Tunapendana na zaidi ya yote sisi ni familia. Tumeliweka hili nyuma na tunatumaini mtu mwingine yeyote pia atafanya hivyo pia.”
Bado tetesi za chanzo cha ugomvi wao zinaelezwa kuwa ni kitendo cha Jay Z kuonekana anakuwa na ukaribu sana na mwanamitindo Rachel Roy kitu ambacho hakikuwafurahisha Beyonce na Solange.
Chanzo kimeliambia New York Daily News kuwa kitu kilichopandisha hasira za Solange zaidi ni pale Jay Z alipotaka kwenda kwenye after party ya Rihanna bila Beyonce na ikaonekana kama ataenda na Rachel Roy.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!