Siku kama ya leo miaka 561 iliyopita sawa na tarehe 29 Mei 1453
ilikombolewa bandari ya Constantine iliyokuwa makao makuu ya Mfalme wa
Roma ya Mashariki na vikosi vya Sultani Muhammad Fatih, mtawala wa dola
ya Othmaniya. Amri ya kwanza iliyotolewa na Muhammad Fatih baada ya
kuudhibiti mji huo ilikuwa ni kudhaminiwa usalama na uhuru wa wakaazi
wake. Mfalme huyo alitoa amri ya kukarabatiwa mji huo na kujengwa
msikiti, ambao leo hii unajulikana kwa jina la Msikiti wa Sultan Ahmed.
Ilipofika mwaka 1930 mji wa Constantine ulibadilishwa jina na kuitwa
Istanbul, na ni miongoni mwa miji muhimu zaidi ya Uturuki ulioko
magharibi mwa nchi hiyo.
---------------------------------------------------------------------------
Miaka 25 iliyopita katika siku kama ya leo, inayosadifiana na tarehe 8
Khordad mwaka 1368 Hijiria Shamsia alifariki dunia Ayatullah Mir Sayyid
Ali Fani Isfahani msomi wa Kiislamu. Alizaliwa katika mji wa Isfahan
mwaka 1294 Hijira Shamsia na alianza kujifunza elimu ya msingi ya
Kiislamu akiwa na miaka 9. Alimu huyo alistafidi na maulama wakubwa na
kufikia daraja ya ijtihad ambapo alihamia Najaf nchini Iraq na kwa muda
wa miaka 30 alifundisha kwenye mji huo masomo ya fikih, usul, ilmul
qalam na akhlaq. Mwaka 1352 Hijria Shamsia alirejea Iran na kuendelea
kufundisha mjini Qum. Miongoni mwa vitabu vya Ayatullah Mir Sayyid Ali
Fani Isfahani ni Dastur Hajj wal Umrah, Fawaid Rijaliyah, Arubain Hadith
na Tafsiri ya Suratul Faatiha.
Siku kama ya leo miaka 61 iliyopita muwafaka na tarehe 29 Mei 1953,
Edmund Hillary mpanda milima kutoka New Zealand na Tenzing Norgay mpanda
milima kutoka Nepal walifanikiwa kufika kilele cha mlima Everest, ambao
ni mlima mrefu zaidi duniani. Mlima wa Everest wenye urefu wa mita
8,848, ni kilele kirefu zaidi cha silsila ya milima ya Himalaya nchini
Nepal. Baada ya Hillary na Norgay kufanikiwa kupanda mlima huo mwaka
1953, makundi mengine ya wapanda milima kutoka katika nchi nyingine
duniani pia yaliweza kukwea kilele cha mlima huo katika miaka
iliyofuata.
Na Siku kama ya leo, miaka 556 iliyopita alifariki dunia huko mjini
Aleppo, Syria Shamsud-Din, faqihi na mfasiri mkubwa wa Waislamu wa zama
hizo. Shamsud-Din alisoma elimu ya fikihi na tafsiri ya Qur'ani kwa Ibn
Hammam, faqihi na msomi mkubwa wa zama hizo. Aidha Shamsud-Din aliandika
vitabu kadhaa katika uwanja wa mafundisho ya Kiislamu. Miongoni mwa
vitabu vya msomi huyo, ni pamoja na kitabu kiitwacho "Al-taqrir wa
al-Ta'abir."
---------------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------------
-------------------------------------------------------------------------------
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!