Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » HUYU NDIE WAZIRI KUTOKA MALAWI ALIYE JIUWAA KWA KUJIPIGA RISASI BAADA YA KUSHINDWA KWENYE UCHAGUZI

HUYU NDIE WAZIRI KUTOKA MALAWI ALIYE JIUWAA KWA KUJIPIGA RISASI BAADA YA KUSHINDWA KWENYE UCHAGUZI

Written By Unknown on Thursday, 22 May 2014 | Thursday, May 22, 2014

Naibu waziri wa serikali za mitaa wa Malawi amejipiga risasi na kujiua nyumbani kwake mjini Lilongwe.
Godfrey Kamanya alikuwa anayegombea kutetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Nzonzi Kusini amejiua alfajiri ya leo katika mojawapo ya vyumba vya nyumba yake iliyopo Area Ten mjini Lilongwe.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali kuu ya Kamuzu mjini humo, na jeshi la polisi litatoa taarifa rasmi ya kifo hicho baada kukamilisha uchunguzi.
Haijajulikana sababu za Kamanya kujiua japokuwa ameacha barua ya maelezo ambayo polisi wataitoa baadae.
Matokeo ya kura bado hayajatangazwa rasmi katika kile kinachosemekana kuwa uchaguzi wenye ushindani mkali sana.
Afisa mkuu wa uchaguzi, amesema kuwa mfumo wa elektroniki umeharibika na maafisa wanatumia matokeo kwa njia ya barua pepe.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi