Jembe la kazi: Yaya Toure ametikisa
kiberiti Man City kwa kudai anataka kuondoka baada ya klabu yake
kushindwa kuthamini siku yake ya kuzaliwa.
MANCHESTER
City yasalimu amri kwa mwafrika Yaya Toure baada ya mkurugenzi wa soka
wa klabu hiyo, Txiki Begiristain kusema atakuwa na mazungumzo ya amani
na kiungo huyo kwa lengo la kumaliza tofauti zao zilizojitokeza siku za
karibuni.
Wakala wa Toure,
Dimitry Seluk aliibua shari jumanne ya wiki hii kwa kusema kuwa kiungo
huyo anaweza kuihama Man city majira ya kiangazi mwaka huu kutokana na
mabingwa hao wapya wa ligi kuu England na mmliki wake Sheik Mansour
kushindwa kuithamini siku yake ya kuzaliwa wakiwa katika ziara ya baada
ya msimu mjini Abu Dhabi wiki iliyopita.
Kuna
taarifa kuwa Seluk anataka kumrejesha Yaya katika klabu ya Barcelona
ambako alihama mwaka 2010 kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 24 na
sasa ni moja ya wachezaji bora kabisa wanaotegemewa na Man City.
|
Dimitri Seluk |
Wakala wa Toure, Dimitri Seluk aliibua shari kwa kusema kuwa kuna uwezekano mkubwa nyota huyo kuondoka Etihad
Tabasamu: Toure kwasasa yupo katika
kambi ya timu ya taifa ya Ivory Coast baada ya ziara ya baada ya msimu
mjini Abu Dhabi na klabu yake ya Man City.
Toure
amefunga mabao 24 katika mechi 49 alizoichezea Man City msimu uliopita
na kukiwezesha kikosi hicho cha Manuel Pellegrini kutwaa ubingwa.
City
wameshikilia msimamo wao kuwa Toure hataondoka kwasababu bado ana miaka
mitatu katika mkataba wake aliosaini miezi 12 iliyopita na unampatia
paundi laki mbili kwa wiki.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!