Rais Barack Obama wa Marekani amesema kuwa ataongeza misaada ya
nchi yake kwa makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na nchi za kigeni
kufanya mauaji dhidi ya maafisa wa serikali na wananchi Syria. Obama
amesema hayo wakati aliopokuwa anahutubia chuo cha kijeshi cha Marekani
huko New York. Amesema, atashirikiana na baraza la Congress la nchi hiyo
kuongeza misaada kwa wanamgambo wa Syria.
Obama amesema hayo huku kukiripotiwa kuwa Washington ina mpango wa kuanza kuwapatia mafunzo ya kijeshi kwa siri wanamgambo hao katika kituo kimja cha kijeshi nchini Qatar kwa lengo la kwenda kuwashambulia askari wa serikali ya Syria. Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyochapishwa na Jarida la Wall Street Journal siku ya Jumanne, wanajeshi wa Marekani wana mpango wa kuwapa mafunzo wanamgambo wanaopigana dhidi ya serikali ya Damascus wanaojiita 'Jeshi la Ukombozi wa Syria.'

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!