Home »
siasa afrika
» KATIBU MKUU WA UN ASEMA KUWA KIONGOZI WA WAASI WA SUDANI KUSINI AMEKUBALI KUKUTANA USO KWA USO NA RAIS WA NCHI HIYO
KATIBU MKUU WA UN ASEMA KUWA KIONGOZI WA WAASI WA SUDANI KUSINI AMEKUBALI KUKUTANA USO KWA USO NA RAIS WA NCHI HIYO
|
Ban Ki moon |
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon, amesema kuwa kiongozi wa
waasi nchini Sudan Kusini, Riek Machar, amekubali kukutana ana kwa ana
na Rais Salva Kiir ili kutatua mgogoro unaoendelea kuikaba koo nchi hiyo
changa zaidi barani Afrika. Ban Ki moon amesema hayo baada ya kufanya
ziara ya siku moja huko Sudan Kusini hapo jana.
|
Riek Machar |
Katibu Mkuu wa UN
ameongeza kuwa, Rais Salva Kiir pia amemuhakikishia kwamba yuko tayari
kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na hasimu wake, Riek Machar mjini
Addis Ababa, Ethiopia. Ziara ya mkuu huyo wa UN nchini Sudan Kusini
imefanyika huku wanajeshi wa serikali na waasi wakiendelea kupigania
udhibiti wa mji muhimu wa Bentiu wenye utajiri mkubwa wa mafuta. Sudan
Kusini ilitumbukia katika vita na machafuko ya ndani Disemba 15 mwaka
jana baada ya Rais Salva Kiir kumtuhumu makamu wake wa zamani, Riek
Machar kuwa alifanya jaribio la kupindua serikali yake
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!