Home »
siasa afrika
» RAIS WA TANZANIA JAKAYA KIKWETE AAHIDI KUIMARIKA KWA USALAMA KASKAZINI MASHARIKI MWA JAMUHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO
RAIS WA TANZANIA JAKAYA KIKWETE AAHIDI KUIMARIKA KWA USALAMA KASKAZINI MASHARIKI MWA JAMUHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO
Rais Jakaya mrisho Kikwete wa Tanzania, ametaka kuimarishwa
usalama na amani katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo. Rais Kikwete ameyasema hayo mjini Kinshasa na kusisitiza kuwa,
kuna haja ya kurejeshwa amani huko mashariki mwa Kongo baada ya
kushuhudiwa machafuko ya muda mrefu ya waasi. Aidha Rais wa Tanzania
ameashiria uhusiano mwema uliopo kati ya Dar es Salam na Kinshasa kwa
kusema kuwa, Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni nchi mbili
zenye ujirani mwema na hivyo akataka kuimarishwa zaidi uhusiano mwema
katika uwanja wa uchumi. Tanzania ni moja ya nchi zenye askari wake
nchini Kongo chini ya mwavuli wa askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda
amani (MONUSCO). Licha ya kundi la M23 moja ya makundi makubwa
yaliyokuwa yakiendesha vita dhidi ya serikali ya Kinshasa kuweka chini
silaha na kujiunga na mwenendo wa amani nchini humo, lakini bado maeneo
ya mashariki mwa taifa hilo la katikati mwa Afrika yanaendelea
kushuhudia machafuko, kutokana na kuwepo wa makundi ya waasi kama vile
Mai-Mai. Rwanda na Uganda ni nchi mbili jirani ambazo zimekuwa
zikinyoshewa kidole cha lawama zikidaiwa kuwaunga mkono waasi dhidi ya
serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!