Jenerali wa zamani wa jeshi la Libya Khalifa Haftar ameanza tena
mashambulizi ya anga dhidi ya mji wa Benghazi ambayo yamezilenga kambi
za wanamgambo kwenye mji huo.
Imeripotiwa kuwa mashambulizi hayo yameratibiwa na kufanywa na askari watiifu kwa jenerali huyo walioasi jeshini.
Haftar alianza kuwashambulia wanamgambo katika mji huo wa Mashariki mwa Libya Mei 15 akisema kuwa, anataka kuwasambaratisha na kuimarisha usalama wa nchi hiyo.
Wakati huo huo watu wenye silaha wameshambulia kikosi cha Wizara ya Mambo ya Ndani kilichopewa jukumu la kulinda serikali ya nchi hiyo. Bunge limelaani shambulizi hilo na kusema kuwa jambo hilo halikubaliki.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!