Zaidi ya watu 60 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya
kutokea miripuko kadhaa ya mabomu nchini Iraq. Miripuko miwili ya
kutegwa garini imetokea katika mji wa kaskazini mwa Iraq wa Mosul ambapo
makumi ya watu wameuawa wakiwemo askari na wahudumu wa afya.
Halikadhalika miripuko kadhaa imelenga mji wa Tuz Khurmatu na kuuawa watu watano, wanne wakiwa wa familia moja. Mripuko mwingine umetokea karibu na eneo la Kadhimiyah mjini Baghdad ambapo watu 16 wameuawa na wengine 50 kujeruhiwa.
Iraq imekuwa ikishuhudia wimbi la machafuko katika miaka ya hivi karibuni. Maafisa wa nchi hiyo wanasema kuwa, zaidi ya watu 1,000 wengi wao wakiwa raia wameuawa na wengine 1,400 kujeruhiwa katika machafuko yaliyojiri nchini humo mwezi uliopita wa Aprili.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!