Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » OXFAM LATOWA TAHADHARI LA NJAA SUDAN KUSINI

OXFAM LATOWA TAHADHARI LA NJAA SUDAN KUSINI

Written By Unknown on Thursday, 15 May 2014 | Thursday, May 15, 2014

Shirika la kimataifa la misaada ya kibinadamu la Oxfam limetahadharisha kuhusu uwezekano wa kuzuka baa la njaa nchini Sudan Kusini.
Mark Goldring Mkurugenzi  Mkuu wa shirika hilo amesema kwamba, katika hali ambayo hakuna dalili zozote za kumalizika mapigano ya umwagaji damu Sudan Kuisni, nchi hiyo iko katika hatari kubwa ya kukumbwa na matatizo makubwa ya ukosefu wa chakula.
Aidha ametaka jamii ya kimataifa ichukue hatua za haraka ili kuzuia kuzuka mgogoro mkubwa wa kibindamu katika nchi hiyo ya Kiafrika.
Ijapokuwa Rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar walisaini makubaliano ya amani wiki iliyopita lakini masaa machache tu baadaye mapigano yalishuhudiwa tena nchini humo.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa zaidi ya thuluthi moja ya wananchi milioni 3.7 wa Sudan Kusini wanahitajia  misaada ya dharura ya chakula.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi