Uchaguzi wa rais wa Misri umerefushwa kwa siku moja zaidi katika
jitihada za kuongeza idadi ya wapiga kura ambayo inahatarisha uhalali wa
uchaguzi huo. Uamuzi huo ulichukuliwa jana usiku baada ya kuonekana
kuwa watu waliojitokeza kwenye zoezi hilo lililokuwa limefanyika kwa
siku mbili mfululizo ilikuwa ndogo sana. Mkuu wa kamisheni ya uchaguzi
wa Misri Abdul Azizi Salman alitangaza kuwa, hadi jana usiku asilimia 37
ya wapiga kura ndio waliojitokeza kati ya Wamisri milioni 53
waliotimiza masharti ya kupiga kura.
Harakati ya Ikhanul Muslimin ambako anatoka rais aliyepinduliwa na jeshi Muhammad Mursi iliwataka wafuasi wake kususia uchaguzi huo. Pia uchaguzi wa rais wa Misri umesusiwa na vijana wanaounga mkono demokrasia ambao walishiriki katika harakati za mapinduzi za mwaka 2011 zilizoangusha utawala wa dikteta Hosni Mubarak.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!