Katibu Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa
Maulamaa wa Kiislamu amesema kuwa, udanganyifu mkubwa umetokea katika
historia ya uchaguzi duniani nchini Misri. Al Qarah Baghi ameeleza kuwa,
kwa mujibu wa ripoti, idadi ya kura zilizoharibika kwenye uchaguzi huo
zilikuwa nyingi zaidi ya kura alizopata mgombea Hamdin Swabahi na kwamba
suala hilo linaonesha kubatilika uchaguzi huo wa Misri.
Wakati huo huo Harakati ya Ikhawanul
Muslimin ya Misri imetangaza kuwa kushiriki kiwango kidogo cha wananchi
kwenye zoezi hilo ni muhuri uliobatilisha siasa za wafanya mapinduzi ya
kijeshi. Harakati hiyo pia imewasifu wananchi wa Misri kwa kususia
uchaguzi huo. Kamisheni ya uchaguzi ya Misri mara ya kwanza ilitangaza
kuwa asilimia 37 ya wananchi wameshiriki kwenye uchaguzi huo. Lakini
baada ya kuongezwa siku moja ya kupiga kura, ilitangazwa kuwa asilimia
44.4 ya Wamisri wameshiriki katika zoezi hilo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!