Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HALI YA MACHAFUKO INAYO ZIDI KUENDELEA KURIPOTIWA SUDAN KUSINI YAITIYA HOFU UMOJA WA MATAIFA(U.N)

HALI YA MACHAFUKO INAYO ZIDI KUENDELEA KURIPOTIWA SUDAN KUSINI YAITIYA HOFU UMOJA WA MATAIFA(U.N)

Written By Unknown on Thursday, 5 June 2014 | Thursday, June 05, 2014

Ban Ki-moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani kuendelea umwagaji damu nchini Sudan Kusini kutokana na kutoheshimiwa makubaliano ya usitishaji vita na kuzitaka pande hasimu za mgogoro wa nchi hiyo kuacha operesheni zote za kijeshi na kushikamana na ahadi za huko nyuma. Ban amesema hayo katika mazungumzo yake ya simu na Rais Salva Kiir wa nchi hiyo. 
Aidha katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  ameelezea wasiwasi wake kutokana na kuendelea uadui ambao ni kinyume na makubaliano ya Januari 23 ya kuacha uadui,  na pia makubaliano ya Mei 9 yaliyotiwa saini kati ya Rais Salva Kiir na makamu wa rais wa zamani wa Sudan Kusini Riek Machar.
Mapigano nchini Sudan Kusini yamepelekea maelfu ya watu kuuawa na zaidi ya watu milioni 1.3 kuwa wakimbizi.
Umoja wa Mataifa huko nyuma ulisema pia kuwa, kuheshimiwa usitishaji mapigano ni muhimu ili kuboresha hali mbaya ya kibinadamu inayoshuhudiwa katika nchi hiyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi