Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HAWA NDO WACHEZAJI WAWILI WA TIMU YA TAIFA YA GHANA AMBAO WAMETEMWA NA MOJA KWA MOJA KUPANDISHWA NDEGE YAKUWAREJESHA MA KWAO MUDA MCHACHE KABLA YAKUUMANA NA URENO.

HAWA NDO WACHEZAJI WAWILI WA TIMU YA TAIFA YA GHANA AMBAO WAMETEMWA NA MOJA KWA MOJA KUPANDISHWA NDEGE YAKUWAREJESHA MA KWAO MUDA MCHACHE KABLA YAKUUMANA NA URENO.

Written By Unknown on Thursday, 26 June 2014 | Thursday, June 26, 2014

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ghana Kwesi Appiah, amefanya maamuzi magumu ya kuwatimua kambini viungo mahiri wa kikosi chake Sulley Muntari na Kevin-Prince Boateng, ikiwa ni muda mchache kabla ya The Black Stars haijashuka dimbani kucheza mchezo wa mzunguuko wa tatu wa kundi la saba dhidi ya timu ya taifa ya Ureno katika michuano ya kombe la dunia inayoendelea huko nchini Brazil.
Muntari, ambaye anaitumikia klabu ya AC Milan ya nchini Italia, pamoja na Boateng, wa klabu ya Schalke 04 ya nchini Ujrumani, wameondolewa kambini na kocha Appiah baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu wakiwa kambini.
Muntari amelazimika kuadhibiwa na kocha, baada ya kumpiga kibao afisa wa chama cha soka nchini Ghana Moses Armah Parker ambae ameongozana na kikosi cha The Black Stars nchini Brazil.

Taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa chama cha soka nchini Ghana GFA imeeleza kwamba mchezaji huyo alifikia hatua ya kumpiga afisa huyo baada ya kupishana nae kauli ikiwa ni dakika chache baada ya kuwekwa kikao mbacho kilifanyika kambini jana jioni.
Hata hivyo mazungumzo kati ya wawili hao yamefanywa kuwa siri, kutokana na sababu za kinidhamu kwa wachezaji waliobaki kambini.
Katika hatua nyingine Appiah, amemuondoa kambini Kevin-Prince Boateng, kufuatia kauli chafu alizozitoa mbele ya kocha huyo mzawa wakati wa mazoezi ya timu ya taifa ya Ghana.
Alipoulizwa juu ya taarifa hizo kama zina ukweli wowote Boateng, aliwathibitishia waandishi wa habari kwa kueleza kwamba ni kweli yu njiani kurejea nyumbani na kuanzia sasa sio sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ghana.


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi