Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza kuwapa msamaha wafungwa wa
kisiasa kutoka makundi mbalimbali ya nchi hiyo. Lambert Mende Omalanga
Waziri wa Habari na Msemaji wa Serikali ya Kongo amesema kuwa, wafungwa
109 wa kisiasa kutoka makundi na harakati mbalimbali za kisiasa wamepata
msamaha huo tokea mwezi Februari mwaka huu. Waziri Omalanga amesema
kuwa wafungwa 9 kutoka kundi la waasi wa zamani wa M23, 21 wanamgambo wa
Batanga-Katanga na wengine 22 wanamgambo waliohusika na shambulio dhidi
ya makazi ya rais tarehe 17 Februari mwaka 2011 ni miongoni mwa
wafungwa waliopata msamaha wa serikali ya Kinshasa. Waziri wa Habari wa
Kongo amesema kuwa, watu waliotenda jinai dhidi ya binadamu na vitendo
vya ubakaji, hawakupata msamaha huo wa serikali ya Kinshasa. Inafaa
kuashiria hapa kuwa, serikali ya Kongo ilitangaza kutoa msamaha baada ya
kusambaratishwa kundi la M23, kwa lengo la kurejesha utulivu na umoja
wa kitaifa nchini humo.
Home »
siasa afrika
» KAMA HAUKUBAHATIKAA BASI HII NDO TAARIFA ILIYO TOLEWA NA SERIKALI YA RAIS KABILA KUHUSU WAFUNGWA WA KISIASA
KAMA HAUKUBAHATIKAA BASI HII NDO TAARIFA ILIYO TOLEWA NA SERIKALI YA RAIS KABILA KUHUSU WAFUNGWA WA KISIASA
Written By Unknown on Monday, 9 June 2014 | Monday, June 09, 2014
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!