Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » KUNDI LA AL-SHABAAB LAKIRI KUHUSIKA KWA SHAMBULIYO LA HIYO MAJUZI HUKO LA LAMU KENYA AMBAPO WATU ZAIDI YA 48 WALIFARIKI DUNIA.

KUNDI LA AL-SHABAAB LAKIRI KUHUSIKA KWA SHAMBULIYO LA HIYO MAJUZI HUKO LA LAMU KENYA AMBAPO WATU ZAIDI YA 48 WALIFARIKI DUNIA.

Written By Unknown on Tuesday, 17 June 2014 | Tuesday, June 17, 2014

Kundi la al Shabab la nchini Somalia limetangaza kuwa limehusika na shambulio lililotokea Lamu, nchini Kenya na kuua watu 48 na makumi ya wengine kujeruhiwa.
Taarifa kutoka Nairobi zinasema kuwa, shambulio hilo lililofanyika katika eneo la Mpeketoni katika pwani ya Kenya, lilitekelezwa na wanamgambo wa kundi hilo. Shambulio hilo limetokea katika hali ambayo, serikali ya Kenya ilitangaza kuwa imara katika kukabiliana na mashambulio ya kigaidi nchini humo.
Kufuatia shambulizi hilo baadhi ya wabunge wa Kenya wanapanga mikakati ya kumsaili na kumtimua kazi Waziri wa Mambo ya Ndani kwa tuhuma za kushindwa kukabiliana na ugaidi.

Inafaa kuashiria hapa kuwa, wanamgambo hao wa al Shabab licha ya kuwafyatulia risasi watu waliokuwa barabarani na mahotelini, walivamia kituo cha polisi na kukiteketeza kwa moto. Wakati huohuo, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Ubelgiji imewatahadharisha raia wake kufanya safari nchini Kenya.


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi