Mshambuliaji kutoka nchini Uruguay Luis Alberto Suárez Díaz,
hatimae ametangaza hadharani taarifa za kutarajia kucheza mchezo wa
kwanza wa kundi la nne, katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2014
huko nchini Brazil.
Luis Suarez alikuwa katika mazingira ya kuzikosa fainali za kombe la dunia za mwaka huu, kufuatia majeraha ya goti ambayo yalibainika siku chache baada ya kujiunga na wachezaji wenzake kambini.
Suarez amethibitisha taarifa za kutarajia kuwa sehemu ya kikosi Uruguay, ambacho kitaanza kampeni ya kuusaka ubingwa wa dunia kwa kucheza dhidi ya timu ya taifa ya Costa Rica katika uwanja wa Castelão, mjini Fortaleza nchini Brazil june 14.
Amesema kwa sasa anajihisi yupo vizuri kiafya tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma hivyo anategemea kama atacheza mchezo dhidi ya Costa Rica kutakuwa na uhakika wa asilimia mia moja kuwakabili Uingereza, katika mchezo wa pili wa kundi la nne ambao umepangwa kucheza June 19 kwenye uwanja wa de São Paulo, mjini São Paulo.
Hata hivyo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, amesema alikuwa anaomba usiku na mchana ili aweze kupona jaraha la goti ambalo lilimpa shaka huenda angezikosa fainali za kombe la dunia za mwaka huu lakini dua zake zimesikika na sasa anajiandaa kuingia uwanjani.
“Ninamshukuru Mungu kwa hali niliyo nayo sasa, nilimuomba kila siku ili niweze kurejea katika afya yangu njema na hii leo sina budi kujipa matumaini ya kutarajia kucheza mchezo wa ufunguzi wa kundi la nne dhidi ya Costa Rica.” Amesema Suarez.
“Pia ninawashukuru wachezaji wenzangu kwani walinipa moyo kwa kuwa na mimi wakati wote wa kuuguza jeraha langu, na nina hakika kurejea kwangu uwanjani kutaendelea kujenga umoja miongoni mwetu na hatimae tutafikia malengo tunayoyakusudia”. Ameongeza mshambuliaji huyo wa klabu ya Liverpool.
Luis Alberto Suárez Díaz, alipata majeraha ya goti wakati wa mchezo wa mwisho wa ligi ya nchini Uingereza msimu wa mwaka 2013-14, ambapo Liverpool walipambana na Newcastle Utd ambao walikubali kupoteza kwa kufungwa mabao mawili kwa moja.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!