Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » ONGEZEKO LA UGAIDI BARANI AFRIKA LAIWEKA WASIWASI UMOJA WA AFRICA (A.U).

ONGEZEKO LA UGAIDI BARANI AFRIKA LAIWEKA WASIWASI UMOJA WA AFRICA (A.U).

Written By Unknown on Tuesday, 24 June 2014 | Tuesday, June 24, 2014

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Bi. Nkosazana Dlamini-Zuma ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuongezeka migogoro na mashambulizi ya kigaidi barani Afrika na kutoa mwito wa kufanyika jitihada zaidi kukabiliana na hali hiyo.
Akizungumza mjini Malabo, huko Equatorial Guinea, kwenye kikao cha Baraza Kuu la AU, Bi. Zuma amelaani mashambulizi ya kigaidi ya hivi karibuni katika nchi za Nigeria, Kenya na Libya akisema kuwa, vita dhidi ya ugaidi vinapaswa kushadidishwa.
Pia amelaani vikali kitendo cha kutekwa nyara zaidi ya wanafunzi 200 wa kike huko Nigeria na kusema kuwa, magaidi wamevuka mstari mwekundu na kwa mantiki hiyo inabidi kupambana nao kwa nguvu zote.
Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika pia amezungumzia migogoro ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini na kukumbusha kuwa, migogoro ni moja kati ya viunzi vinavyozuia ukuaji wa uchumi barani Afrika.
Amesema AU pamoja na jumuiya zingine za kikanda zinapaswa kushirikiana ili kutatua migogoro hiyo miwili inayotishia mustakabali wa kiuchumi na kiusalama barani Afrika.


 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi