Raia wa utawala haramu wa Israel amefikishwa mahakamani nchini
Kenya akikabiliwa na mashtaka ya kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi la
al-Shabab.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la nchini Kenya, Muisraeli huyo anayetambulika kwa majina ya Jabareen Ahmed na Harum Osama na mshukiwa mwenza Mohammad Salim kutoka Morocco walikamatwa mwezi Februari wakijaribu kutekeleza hujuma za kigaidi nchini Kenya.
Katika kesi iliyosikilizwa jana mjini Nairobi, raia huyo wa utawala haramu wa Israel amebainika kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi la al Shabaab na alikuwa na nyaraka zilizoonyesha namna alivyopanga kutekeleza hujuma za kigaidi nchini Kenya. Maafisa wa kitengo cha kupambana na ugaidi Kenya wanasema gaidi huyo raia wa Israel alipatikana na video yenye maelezo kuhusu mbinu ya CIA ya kutengeneza mabomu ambayo alitaka kutumia kutekeleza ugaidi.
Washukiwa hao walifikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali na wataendelea kushikiliwa hadi kesi yao iamuliwe. Kesi hiyo inatazamiwa kuendelea Juni 18. Kenya imekumbwa na hujuma za kigaidi katika miezi ya hivi karibuni na wafuasi wa muungano unaotawala wa Jubilee wanasema hujuma hizo ni sehemu ya njama za nchi za Magharibi za kuiangusha serikali hiyo kwa sababu ya sera zake huru za kushirikiana zaidi na nchi za Mashariki hasa China.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!