Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » SERIKALI YA RAIS JAKAYA KIKWETE YAANDAMWA KWA HALI YA JUU NA VYAMA VYA UPINZANII

SERIKALI YA RAIS JAKAYA KIKWETE YAANDAMWA KWA HALI YA JUU NA VYAMA VYA UPINZANII

Written By Unknown on Thursday, 5 June 2014 | Thursday, June 05, 2014

Vyama vya upinzani nchini Tanzania vimezidi kuisakama Serikali vikisema kuwa hivi sasa kila mtanzania ana deni la Shilingi 600,000 kutokana na fedha zilizokopwa kuendeshea warsha, semina, safari, mafunzo na matengenezo ya magari.
Vyombo vya habari nchini Tanzania vimemnukuu Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia akiwasilisha taarifa ya kambi ya Upinzani bungeni na kusema kuwa, deni la taifa limeongezeka kwa Shilingi trilioni 8.2 kwa kipindi cha miezi saba tu na kwamba ukiligawanya deni hilo kwa idadi ya Watanzania milioni 45, kila mwananchi atakuwa anadaiwa Shilingi laki sita (600,000).
 Vyombo hivyo vimeongeza kuwa, karibu fedha zote zilizotengwa na Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha wa 2014/15, zitatumika katika kulipia Deni la Taifa. Vimesema, kati ya Shilingi trilioni 5.8 za bajeti ya Wizara ya Fedha mwaka 2014/15, Shilingi trilioni 4.3 zimetengwa kwa ajili ya kulipia Deni la Taifa.
Wapinzani hao pia wamesema, ingawa serikali ya Tanzania inasema kuwa deni hilo linavumilika, lakini linaonekana kuwaelimia Watanzania kwani hata mapato ya ndani yamezidiwa na matumizi ya kawaida hivyo kuifanya Serikali kukopa hata kwa ajili ya warsha, semina, safari, mafunzo na matengenezo ya magari.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi