Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » SIRI YAFICHUKAA KUMBE,SUAREZ KUMBE ALIKUWA NA PLAN ZAKUMNGATA MENO G.CHIELLINI TOKA MWAKA 2013.

SIRI YAFICHUKAA KUMBE,SUAREZ KUMBE ALIKUWA NA PLAN ZAKUMNGATA MENO G.CHIELLINI TOKA MWAKA 2013.

Written By Unknown on Thursday, 26 June 2014 | Thursday, June 26, 2014



Wakati kamati ya nidhamu ikitarajiwa kufanya maamuzi kufuatia sakata la mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay Luis Alberto Suarez Diaz, ambae anatuhumiwa kumng’ata beki wa timu ya taifa ya Italia Giorgio Chiellini, vyombio vya habari vimeendelea kuliongezea chumvi sakata hilo.
Licha ya shirikisho la soka duniani FIFA kuvitaka vyombo vya habari kuwa na subra, bado imeonekana ombi hilo linakiukwa kutokana na picha zaidi kuendelea kutolewa kama vielelezo vya kuishurutisha kamati ya nidhamu kumchukua hatua kali Luis Suarez.
Mapema hii leo baadhi ya mitandao wamekumbushia kitendo kwa njia ya picha, ambacho kilitokea miezi kumi na mbili iliyopita ambapo Uruguay walikutana na Italia kwenye michuano ya kombe la mabara iliyofanyika nchini Brazil.
Katika picha hiyo inadaiwa Luis Suarez aliwahi kujaribu kumng’ata Giorgio Chiellini, lakini zoezi hilo lilishindikana kutokana na umbali wa sentimita chache uliokuwepo baina ya wawili hao.
Hatua hiyo inachukuliwa kama chuki iliyojengeka kati ya vyombo vya habari dhidi ya Luis Suarez, ambaye hakuwahi kuzungumzwa vibaya mara tu, zoezi hilo liliposhindikana mwaka 2013, lakini hii leo inachukuliwa kama kigezo cha kuisisitiza kamati kwa kuonyesha huenda mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amezaea kufanya hivyo.
Jana mchana vyombo vya habari hususan vya Uingereza, vilishinikiza adhabu kali itolewe dhidi ya Luis Suarez na kama itakuwa kwa uchache basi aadhibiwe kwa kufunguwa michezo 24 na ikiwezekana afungiwe kucheza soka kwa kipindi cha miaka miwili.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi