Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » TAARIFA KUTOKA UINGEREZA ZASEMA KUWA RATIBA YA MICHEZO YA LIGI KUU YA SOKA YA B.P.L IMEVUJAA SIKU MOJA KABLA.

TAARIFA KUTOKA UINGEREZA ZASEMA KUWA RATIBA YA MICHEZO YA LIGI KUU YA SOKA YA B.P.L IMEVUJAA SIKU MOJA KABLA.

Written By Unknown on Tuesday, 17 June 2014 | Tuesday, June 17, 2014

Baadhi ya vyombo vya habari nchini Uingereza vimetoa taarifa za kuvuja kwa ratiba ya ligi kuu ya soka nchini humo ambayo inatarajiwa kutolewa hapo kesho na chama cha soka FA.
Mitandao mbali mbali ya habari nchini Uingereza imeonyesha ratiba hiyo ambayo kwa sasa inaendelea kupangwa na FA lakini maswali kadha wa kadha yamekuwa yakiwaumuza vichwa mashabiki wa soka nchini humo kwa kujiuliza kama ratiba hiyo iliyovuja ina ukweli ama imetengenezwa na baadhi ya mashabiki.
Ratiba hiyo inaonyesha michezo ya ufunguzi wa ligi ya nchini Uingereza msimu wa mwaka 2014-15 itashuhudia mabingwa watetezi Man City wataanzia nyumbani Etihad Stadium kwa kucheza dhidi ya Southampton.
Aston Villa ambao wapo chini ya Meneja Paul Lambert watawakatibisha Man Utd huko Villa Park wakiwa na meneja wao mpya Louis van Gaal.
Ratiba hiyo iliyozua utata pia inaonyesha Chelsea wataanzia nyumbani Stamfod Bridge kwa kupambana na Everton mnamo August 15, huku mabingwa wa kombe la FA Arsenal wakipangiwa kuanza ugenini kwa kuwakabili Liverpool ambao watakuwa mbele ya mashabiki wao huko Anfield.
Tottenham Hotspurs watabaki nyumbani White Hart Lane kuwakabili Leicester city waliorejea katika ligi ya nchini Uingereza baada ya miaka kumi.
Hata hivyo mashabiki wa soka duniani kote hawana budi kusubiri ratiba ya ligi ya nchini Uingereza msimu wa mwaka 2014-15 ambayo imepangwa kuwekwa hadharani June 18.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi