Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Misri Nabil Fahmi amekutana
katika nyakati tofauti na mawaziri wenzake wa Ethiopia, Tanzania na
Angola mjini Cairo na kujadiliana nao kwa kina masuala yanayohusiana na
pande mbili na nchi zote zinazopakana na Mto Nile.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Misri amesema kuwa,
mazungumzo hayo yamefanyika mjini Cairo wakati mawaziri hao
waliposhiriki sherehe za kuapishwa Rais Abdulfattah al Sisi wa Misri.
Badr Abdul'Atwii amesema kuwa, mazungumzo ya mawaziri hao yalisisitiza
juu ya kubakia Mto Nile kama msingi wa mashirikiano ya nchi zote
zinazochangia maji ya mto huo na kutafutwa njia zitakazozinufaisha nchi
zote kwa maji ya mto huo bila ya kuathiri maslahi ya upande mwingine.
Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania, Ethiopia na Angola
wamesisitiza suala la kurejeshwa uanachama wa Misri kwenye Umoja wa
Afrika hasa baada ya kufanyika uchaguzi wa rais nchini humo.
Misri na Ethiopia zinavutana kuhusiana na matumizi ya maji ya Mto
Nile, baada ya serikali ya Addis Ababa kuchukua uamuzi wa kujenga bwawa
pambizoni mwa mto huo, hatua ambayo inapingwa mno na Cairo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!