Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , , » NEYMAR AONESHA MOYO WA UPENDO KWA KUMSAMEHE YULE MCHEZAJI WA COLOMBIA ALIYETAKA KUMSABABISHIA ULEMA.

NEYMAR AONESHA MOYO WA UPENDO KWA KUMSAMEHE YULE MCHEZAJI WA COLOMBIA ALIYETAKA KUMSABABISHIA ULEMA.

Written By Unknown on Friday, 11 July 2014 | Friday, July 11, 2014

Mshambuliaji wa kutumainiwa wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar da Silva Santos JĂșnior amejikuta akibugujikwa na machozi, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya hali yake mara baada ya kupata majeraha ya mgongo mwishoni mwa juma lililopita.
Neymar amekutana na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu aliporuhusiwa kutoka hospitalini ambapo alikuwa akipatiwa matibabu ya kufuatia jeraha la mgongo ambalo liliwashtua mashabiki wengi wanaozifuatilia fainali za kombe la dunia.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amesema alikuwa hatarini kupoza, kutokana na kubainika wazi kwamba endapo Juan Zuniga angemjeruhi sentimita chache kwenda chini angepata kilema cha maisha.
Mshambuliaji huyo aliyefunga mabao manne kabla ya kuumia wakati wa mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Colombia, pia amesema beki wa The Coffers, Juan Zuniga amempigia simu na kumuomba radhi kwa kumfanyia rafu mgongoni kwenye mchezo huo.
Wakati akizungumzia suala hilo Neymar akijikuta akibugujikwa na machozi.


"Zuniga alinipigia simu siku chache baadaye kuniomba msamaha na kuniambia kwamba hakudhamiria kuniumiza," amesema Neymar. "Nimeukubali msamaha huu, lakini siwezi kulichukulia lile kama tukio la kawaida. Siwezi hata kusema lilikuwa tukio la makusudi, lakini kila mmoja anafahamu haikuwa kawaida. Namna alivyokuja, nyuma yangu, nisingeweza kujitetea.
"Namshukuru Mungu kanisaidia, kwa sababu kama pigo lile lingezama ndani kwa inchi chache, ningeweza kupooza,"amesema Neymar huku akibubujikwa na machozi.
Neymar amesema hajui nini tatizo hadi Brazil ikafungwa 7-1 katika mchezo wa hatua ya nusu fainali na Ujerumani.
"Kilichotokea hakikutarajiwa. Lakini hata walipokuwa nyuma kwa 6-0, 7-0, hawakukata tamaa, waliendelea kukimbia, kuendelea kujaribu.
Sioni aibu kuwa Mbrazil, sioni aibu kuwa sehemu ya timu hii.
Ninajivunia kila mmoja katika wachezaji wenzangu,"amesema.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi