Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya jana aliwaalika katika dhifa ya futari
mabalozi Waislamu walio nchini humo wakiwakilisha nchi za Kiislamu za
Afrika, Asia na Mashariki ya Kati. Katika dhifa hiyo iliyofanyika katika
Ikulu ya Rais mjini Nairobi, Rais Kenyatta alisema Kenya inaweza
kujifunza mengi kutoka nchi za Kiislamu kwani zinakabiliana na
changamoto ambazo hivi sasa Kenya inakabiliana nazo. Alisema ugaidi na
vijana kupewa mafunzo yenye misimamo mikali ni changamoto kubwa katika
maelewano ya kitaifa. Rais Kenyatta amesema kuna haja ya Wakenya na
jamii ya kimataifa kuungana kupambana na ugaidi na vitendo vingine vya
uhalifu ambavyo vimechukua sura ya kimataifa. Katika kikao hicho, Rais
wa Kenya aliunga mkono pendekezo la kuundwa jopo la mabalozi Waislamu
ambao watashirikiana na serikali yake katika kukabiliana na changamoto
zinazoikabili nchi hiyo. Balozi wa Morocco nchini Kenya Bw. Abdelilah
Benryane ambaye alizungumza kwa niaba ya mabalozi wenzake alimhakikishia
Rais Kenyatta kuwa wamekutana baada ya kubaini kuwa changamoto za
usalama zinahitaji umoja na ushirikiano. Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu
ya Iran nchini Kenya Bw. Malik Hussein Givzad ni kati ya wanadiplomasia
wa nchi za Kiislamu walioshiriki katika dhifa hiyo ya futari.
Picha hizi hapa na yeye pia akitupia kilemba shingoni:
Picha hizi hapa na yeye pia akitupia kilemba shingoni:
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!