Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi UNHCR limeiomba jamii ya
kimataifa kuwasaidia wakimbizi wa Sudan Kusini. UNHCR imesema inahitaji
msaada wa dola milioni 658 kwa minajili ya kuwasaidia wakimbizi wa Sudan
Kusini. Ripoti zinasema kuwa, mapigano yaliyotokea katika nchi hiyo
yamesababisha mgogoro wa kibinadamu nchini humo kuwa mbaya zaidi, na
kuwalazimisha mamia ya maelfu ya raia kukimbilia nchi jirani zikiwemo
Kenya, Ethiopia, Sudan na Uganda. UNHCR imetangaza kuwa, hivi sasa kuna
wakimbizi laki saba na elfu kumi na tano, ambapo karibu asilimia 94 ya
wakimbizi hao ni wanawake na watoto.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, nchi changa ya Sudan Kusini ambayo ilijipatia uhuru wake miaka mitatu iliyopita, ilianza kutumbukia kwenye machafuko mwezi Disemba mwaka jana, baada ya majeshi ya serikali ya Juba kupambana na wanamgambo waasi wanaoongozwa na Riek Machar makamu wa zamani wa rais wa nchi hiyo. Hata hivyo, juhudi za Jumuiya ya Kieneo ya IGAD za kurejesha amani nchini humo zilifanikiwa kwa kiasi fulani, baada ya Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na hasimu wake Riek Machar kukubali kutia saini makubaliano ya kusitisha vita nchini humo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!