Umoja wa Mataifa na Marekani zimetangaza kuwa, Harakati ya Kiislamu ya
Palestina Hamas na utawala pandikizi wa Kizayuni wa Israel, zimekubali
kusitisha mapigano kwa muda wa masaa 72, kuanzia asubuhi ya leo Ijumaa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry amenukuliwa akisema kuwa,
kuanzia leo asubuhi kwa nyakati za eneo la Ghaza, kutaanza kusitishwa
vita na kisha Wazayuni na Wapalestina watakwenda mjini Cairo, Misri kwa
minajili ya kuanza mazungumzo. Hata hivyo akizungumza kwa pamoja na Ban
Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kerry amesema kuwa katika
kipindi hicho cha usitishaji vita askari wa Kizayuni walioko katika
maeneo ya vita wataendelea kubakia katika maeneo hayo. Aidha ripoti hiyo
imesisitiza kuwa, ni lazima kuchungwa kikamilifu haki za raia katika
kipindi hicho. Kwa mara kadhaa pande mbili zimekuwa zikiweka makubaliano
ya usitishaji vita, hata hivyo utawala wa Kizayuni umekuwa ukivunja
makubaliano hayo kwa kutumia kwa visingizio tofauti na kuanza
kushambulia kikatili maeneo ya raia katika Ukanda wa Ghaza.
Home »
siasa kimataifa
» HATIMAYE KUNDI LA HAMAS NA SERIKALI YA ISRAEL ZIMEAFIKIANA KUSIMAMISHA MAPIGANO HUKO GHAZA MASAA 72.
HATIMAYE KUNDI LA HAMAS NA SERIKALI YA ISRAEL ZIMEAFIKIANA KUSIMAMISHA MAPIGANO HUKO GHAZA MASAA 72.
Written By Unknown on Friday, 1 August 2014 | Friday, August 01, 2014
Labels:
siasa kimataifa
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!