Real Madrid ambayo ilikuwa na utofauti wa point 6 dhidi ya FC Barcelona, imeikaribisha Getafe katika dimba la Santiago Bernabeu
na kuifunga jumla ya goli 4-1 na kufanya itimize jumla ya point 30 na
michezo 14 ikiwa ni tofauti ya point tatu dhidi ya wapinzani wao wa jadi
FC Barcelona.
Magoli ya Real Madrid yalianza kufungwa na Karim Benzema dakika ya 4 na 16, Gareth Bale dakika ya 35 kabla ya Cristiano Ronaldo kufunga goli la nne dakika 38. Getafe
walirudi kipindi cha pili kutafuta magoli ya kusawazisha, jitihada
ambazo ziligonga mwamba na kuambulia goli moja pekee lililofungwa na Alexis dakika ya 70.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!