
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia amesisitiza juu ya kurejesha amani
huko Somalia. Tedros Adhanom Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia amesema
Addis Ababa inasisitiza kuendelezwa jitihada zilizokwishaanzishwa kwa
ajili ya kurejesha amani na utulivu nchini Somalia. Adhanom amesisitiza
kuwa kuna ulazima wa kurejeshwa amani na utulivu na kuzingaiwa maslahi
ya wananchi wa Somalia. Amesema Ethiopia inaunga mkono kuimarisha
uhusiano kati ya nchi hiyo na Somalia. Waziri wa Mambo ya Nje wa
Ethiopia ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Rais Hassan Sheikh
Mahmoud wa Somalia huko Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia. Katika
mazungumzo hayo Rais wa Somalia amesema pia kuwa Ethiopia imekuwa na
nafasi muhimu katika kusogeza mbele mwenendo wa kusaka amani huko
Somalia. Rais Hassan Sheikh Mahmoud wa Somalia amepongeza pia juhudi za
Addis Ababa katika kuboresha uhusiano wa nchi za Pembe ya Afrika na
kustawisha sekta za biashara na uchumi katika eneo hilo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!