MREMBO, Daniela Saurwald, ambaye ni mchumba wake hakuwepo
hospitali sawa, lakini mama mzazi, Nancy, hakutaka kabisa kusubiri
nyumbani.
Aliandamana na mumewe, Jorge, kumsindikiza mtoto
wao Hospitali ya Northwestern Memorial huko Marekani. Daktari wa Real
Madrid, Carlos Diez, alikuwepo na mwenzake wa timu ya taifa ya
Argentina, Daniel Martinez, naye alikuwapo. Ni kutokana na uzito wa
tatizo lililokuwa likimkabili mtu wao.
Daktari Fessler, ndiye aliyehusika kumpasua. Huyu
ni Gonzalo Higuain, aliyelazimika kufanyiwa upasuaji misimu mitatu
iliyopita kutokana na maumivu ya mgongo yaliyokuwa yakimsumbua na
kutishia uhai wa soka lake.
Uzito wa maradhi yake ndio ulisababisha familia
nzima ya Gonzalo kumsindikiza hospitali. Kocha Jose Mourinho
akishinikiza afanyiwe upasuaji kwa sababu alimwonea huruma kutokana na
hatima ya maisha ya soka la staa huyo wa Kiargentina walipokuwa pamoja
Real Madrid.

Agosti mwaka huu, Real Madrid, ilifanya kufuru
baada ya kuvunja benki na kuandika historia mpya kwenye soka kwa kufanya
usajili wa pesa nyingi zaidi duniani. Ni wakati walipomnasa winga wa
Wales, Gareth Bale, kwa uhamisho wa Paundi 85 milioni.
Uhamisho ulikuwa gumzo Ulaya nzima na kuwafanya
watu wengine wafike mbali na kuchambua mambo mengine ambayo yangeweza
kufanywa kwa kutumia pesa hiyo ya usajili wa Bale.

Daktari asema Real Madrid imeliwa
Katika kusaka ukweli wa kitaalamu kuhusiana na
maradhi ya mgongo yanayomsumbua Bale, gazeti maarufu jijini Madrid,
MARCA lilifanya mahojiano na madaktari mbalimbali mahiri wa
Kihispaniola.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!