
Hivi karibuni wapiganaji wa kikristo wanaomuunga mkono rais aliyepinduliwa madarakani Francois Bozize wamekuwa wakiendesha vitendo vya mauaji dhidi ya wapiganaji wa kiislamu wa Seleka ambao baadhi yao wamejitenga na rais Michel Djotodia.
Katika hatua nyingine nchi ya Rwanda imeungana na Umoja wa Afrika katika kutuma wanajeshi zaidi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kusaidia kuleta amani kwenye taifa hilo ambalo kwa majuma kadhaa hivi sasa limeshuhudia machafuko makubwa.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Rwanda, Louise Mushikiwabo amethibitisha nchi yake kutuma wanajeshi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati huku akishindwa kuweka wazi idadi kamili ya wanajeshi ambao wamepelekwa nchini humo.
Hapo jana pia wanajeshi kutoka nchini Burundi waliwasili kwenye mji mkuu wa taifa hilo Bangui kuungana na wanajeshi wengine wa Umoja wa Afrika walioko nchini humo.
Mpaka sasa idadi ya wanajeshi wa Umoja wa Afrika walioko nchini humo watafikia elfu 6 kuungana na wanajeshi zaidi ya elfu moja na mia sita wa Ufaransa ambao tayari wako nchini humo kutoa usalama kwa raia.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!