Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HATIMAYE WAASI WA RENAMO WA HUKO MSUMBIJI WAREJESHA AMANI KWA KUWEKEANA SAINI YA KUSIMAMISHA MAPIGANO NA SERIKALI YA MAPUTO.

HATIMAYE WAASI WA RENAMO WA HUKO MSUMBIJI WAREJESHA AMANI KWA KUWEKEANA SAINI YA KUSIMAMISHA MAPIGANO NA SERIKALI YA MAPUTO.

Written By Unknown on Monday 25 August 2014 | Monday, August 25, 2014

Amani na utulivu vimerejea sasa huko Msumbiji baada ya mapigano ya miaka miwili kati ya serikali ya Msumbiji na wapinzani. Serikali ya Msumbiji  na chama kikuu cha upinzani cha Renamo jana vilisaini makubaliano ya kusimamisha mapigano. Jose Pacheco Waziri wa Kilimo wa Msumbiji ambaye ni afisa mwandamizi katika timu ya mazungumzo ya serikali na Saimone Macuiana mwakilishi wa timu ya mazungumzo kwa upande wa waasi wa Renamo jana walisaini makubaliano ya kusitisha mapigano baada ya mazungumzo ya masaa sita.
Afisa mwandamizi wa timu ya mazungumzo ya waasi wa Renamo amesema kuwa kutiwa saini makubaliano hayo ni sawa na kumalizika uhasama kati ya Renamo na serikali ya Maputo. Macuiana ameongeza kuwa, ukurasa mpya umefunguliwa huko Msumbiji kwa kufikiwa makubaliano hayo na kwamba nchi hiyo hiyo imeingia katika kipindi kipya. Itakumbukwa kuwa chama tawala cha nchini Msumbiji Frelimo na chama cha upinzani Renamo tarehe 11 mwezi Agosti mwaka huu vilisaini makubaliano ya awali huko Maputo mji mkuu wa nchi hiyo kwa lengo la kukomesha machafuko nchini humo.


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi