Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » JE,ULISIKIA KILE ALICHO KISEMA MKUU WA MONUSCO KUHUSIANA NA WAASI WA KIHUTU WA FDLR? HIKII HAPA.

JE,ULISIKIA KILE ALICHO KISEMA MKUU WA MONUSCO KUHUSIANA NA WAASI WA KIHUTU WA FDLR? HIKII HAPA.

Written By Unknown on Monday 18 August 2014 | Monday, August 18, 2014

Mkuu wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(Monusco) hajapinga uwezekano wa kutumiwa njia ya kijeshi dhidi ya waasi wa Rwanda wa FDLR huko mashariki mwa nchi hiyo. Martin Kobler amesema amewataka waasi wa Rwanda kujiunga kwa khiari na mchakato wa kuweka chini silaha zao. Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa kikosi cha kulinda amani cha umoja huo(Monusco) na jeshi la Kongo vitalazimika kutumia njia ya kijeshi iwapo ombi hilo kwa waasi wa FDLR halitatekelezwa. 
Wakiwa mkutano huko Angola wiki iliyopita,wakuu wa nchi za eneo za Maziwa Makuu ya Afrika pia walitaka kupokonywa silaha waasi hao wa Rwanda na kukaribisha kurejea nchini kwao baadhi ya waasi hao.
Mwenendo wa kuwapokonya silaha waasi wa Rwanda wa FDLR ulianza tarehe 30 mwezi Mei mwaka huu chini ya usimamizi wa jamii ya kimataifa,Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(Sadc).



TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi