Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HABARI KUTOKA SOMALIA ZASEMA KUWA KIONGOZI MUHIMU WA MAHARAMIA AMENASWAA.

HABARI KUTOKA SOMALIA ZASEMA KUWA KIONGOZI MUHIMU WA MAHARAMIA AMENASWAA.

Written By Unknown on Wednesday 20 August 2014 | Wednesday, August 20, 2014

Vikosi vya usalama vya Somalia vimemtia mbaroni mmoja wa viongozi wa maharamia wa nchi hiyo wenye nguvu, ambaye alikuwa akiziteka nyara meli kubwa katika pwani ya Somalia. Kiongozi huyo wa maharamia wa Somalia alikuwa akijipatia mamilioni ya dola kupitia fedha alizokuwa akilipwa kama kikomboleo. Duru za usalama za nje na za ndani ya Somalia zimetangaza kuwa vikosi vya usalama vya Somalia jana usiku vilimtia mbaroni Mohamed Garfanji pamoja na walinzi wake kadhaa huko Mogadishu mji mkuu wa nchi hiyo.
Rais Hassan  Sheikh Mahmoud  wa Somalia mwaka jana alitoa msamaha kwa maharamia wa nchi hiyo ili kukomesha mashambulizi yao karibu na pwani ya nchi hiyo ya eneo la Pembe ya Afrika, hata hivyo  alisema kuwa msamaha huo hauwahusu viongozi wa mtandao huo. Imeelezwa kuwa Mohamed Garfanji amekamatwa katika oparesheni moja ya upokonyaji silaha na kwamba ametiwa mbaroni si kwa sababu ya uharamia. 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi