Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » WATU 1,229 NDIO TAYARI WAMESHA FARIKI HUKO MAGHARIBI MWA AFRIKA KWA AJILI YA HOMA YA EBOLA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI W.H.O YASEMA.

WATU 1,229 NDIO TAYARI WAMESHA FARIKI HUKO MAGHARIBI MWA AFRIKA KWA AJILI YA HOMA YA EBOLA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI W.H.O YASEMA.

Written By Unknown on Wednesday 20 August 2014 | Wednesday, August 20, 2014

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na maradhi hatari ya Ebola katika nchi nne za magharibi mwa Afrika imefikia 1229. WHO limesema kuwa idadi hiyo ya vifo imeongezeka kati ya Agosti 14 hadi 16 mwaka huu, muda ambao ulisajili kesi mpya 113 za Ebola. Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) imesema kuwa mripuko wa homa ya ebola unaenea kwa kasi kuliko vile serikali zinavyoweza kukabiliana na maradhi hayo na kwamba itachukua muda wa miezi sita kuudhibiti ugonjwa huo.
Shirika la Afya Duniani juzi lilizitaka nchi zilizoathiriwa na maambukizo ya homa hatari ya Ebola kuwachunguza wasafiri wote  katika viwanja vya ndege, bandari na vivuko vya nchi kavu wanaosafiri nje ya nchi. Hadi sasa hakuna tiba ya ugonjwa wa Ebola, homa ambayo huambatana na dalili za mtu kuhara, kutapika na kutokwa na damu. Guinea, Liberia na Sierra Leone zimeathiriwa vibaya na homa ya Ebola ambayo sasa hivi pia imeingia huko Nigeria.  
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi