Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » ACHANA NA MARIO BALOTELLI,KAMA ULIKUWA HAUJUI BASI HIZI NDIZO PESA ANAZO IINGIZIA KLABU YAKE YA SASA YA LIVERPOOL KWA SIKU.

ACHANA NA MARIO BALOTELLI,KAMA ULIKUWA HAUJUI BASI HIZI NDIZO PESA ANAZO IINGIZIA KLABU YAKE YA SASA YA LIVERPOOL KWA SIKU.

Written By Unknown on Thursday 11 September 2014 | Thursday, September 11, 2014

Mtendaji mkuu wa klabu ya Liverpool Ian Ayre amepasua ukweli wa mambo baada ya klabu hiyo kufanikiwa kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Italia Super Mario Barwuah Balotelli.Ayre amesema baada ya kukamilisha usajili wa Balotelli akitokea Ac Milan klabu ya Liverpool ilinufaika kwa kuingia kiasi cha paund elfu 50 ambazo zilitokana na mauzo ya jezi yake ambayo ina namba 45.
Ayre amesema kiasi hicho cha pesa kilipatikana kwa siku moja, mbali na mauzo ambayo wanaendelea kuyafanya mpaka hii leo ambapo mashabiki wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye maduka ya klabu hiyo.Amesema pamoja na mauzo hayo kuendelea kufanywa, uongozi wa Liverpool haukumsajili mshambuliaji huyo kwa kutaka kufanya biashara na badala yake walifanya hivyo kwa lengo la kuona soka linachezwa pamoja na kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Luis Alberto Suarez Diaz aliyetimkia nchini Hispania kwenye klabu ya Barcelona.

Super Mario Barwuah Balotelli tangu aliposajiliwa na klabu ya Liverpool tayari ameshaitumikia klabu hiyo katika mchezo mmoja wa ligi ya nchini Uingereza dhidi ya Spurs na majogoo wa jiji walipata ushindi wa mabao matatu wakiwa ugenini huko White Hart Lane. 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi