Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » NCHI YA SUDAN KUSINII YATAADHARISHWA KWA UHABAA WA CHAKULA.

NCHI YA SUDAN KUSINII YATAADHARISHWA KWA UHABAA WA CHAKULA.

Written By Unknown on Thursday 11 September 2014 | Thursday, September 11, 2014

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu imetahadharisha juu ya uhaba wa chakula nchini Sudan Kusini. Mkuu wa kamati hiyo Eric Marclay amesema kuwa, sambamba na kuongezeka utapiamlo , wakimbizi na ukosefu wa huduma za afya vimewafanya wananchi wa Sudan Kusini wataabike mara dufu na matokeo yake hali ya kibinadamu ni mbaya mno.  Ameongeza kuwa, kunahitajika msaada wa haraka wa dola milioni 19 kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wananchi wa nchi hiyo.
Wakati huo huo Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu imesema kuwa, kuhama malaki ya watu huko Sudan Kusini ambao wengi wao bado wanaishi kwenye kambi za muda na kusambaa baadhi yao katika maeneo ya mbali kumewafanya washindwe kufanya kazi na hivyo kuhitajia misaada.  Ripoti zinasema kuwa, utapiamlo unashuhudiwa kwa wingi miongoni mwa watoto nchini Sudan Kusini.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi