Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , , » BAADA YA DIAMOND KUNUSURIKA KUPATA KIPIGO KUTOKA KWA RAIA NA KUKUOKOLEWA NA POLISI WA HUKO UJERUMANI,KWA MARA YA KWANZA SOMA ALICHO KISEMA HAPA.

BAADA YA DIAMOND KUNUSURIKA KUPATA KIPIGO KUTOKA KWA RAIA NA KUKUOKOLEWA NA POLISI WA HUKO UJERUMANI,KWA MARA YA KWANZA SOMA ALICHO KISEMA HAPA.

Written By Unknown on Tuesday 2 September 2014 | Tuesday, September 02, 2014

Polisi nchini Ujerumani wamemnusuru Diamond kutoka kwenye mikono ya mashabiki wenye hasira waliochukizwa na kitendo cha mwimbaji huyo kufika ukumbini saa kumi alfajiri badala ya saa nne usiku kama walivyotarajia, wikendi iliyopita.
Kwa mujibu wa habari kutoka Ujerumani, mashabiki hao waliokuwa na hasira za kusubiri usiku mzima ujio wa Diamond jukwaani waligeuka mbogo alipoingia ukumbini hapo akiwa na promota M-nigeria aliyempeleka na hivyo wakaavamia jukwaa na kuanza kutembeza kipigo kizito kwa ma-DJ na baadhi ya watu waliokuwa wanahusika.
Hali ilivyokuwa ndani ya ukumbi baada ya vurugu

Taarifa hizo zinaeleza kuwa DJ Drazee alipewa kipigo kikali na kupelekwa na kupelekwa hospitali pamoja na DJ mwingine wa kike ‘DJ Flor’ ambaye alipata mshituko wa moyo.
Mashabiki hao walivunja vitu mbalimbali katika ukumbi huo ikiwa ni pamoja na vyombo vya muziki ambavyo vinaelezwa kuwa vilikuwa vibovu (havina ubora).
Polisi wanamsaka muandaaji wa show hiyo huku wakiendelea kuchunguza thamani ya hasara zilizosababishwa na vurugu hizo lakini pia watamfungulia mashtaka promota Britts ambaye ni raia wa Nigeria.
Polisi wakiwa nje ya ukumbi

Kupitia Instagram, Diamond ameandika ujumbe kuhusu tukio hilo na kulitolea ufafanuzi.
“kiukweli nimesikitishwa sana na uandaaji wa kampuni hii ya BRITTS EVENTS iliyoandaa show ya Stuttgart Germany, Promoter anatupeleka kwenye show saa kumi alfajiri. Naomba mtambue halikua kosa langu, mimi ni mgeni tu na ninafata maelekezo ya Promoter hivyo nisingeweza kujiamulia kuja muda ninaotaka mimi."
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi