Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » MJI WA KUDAY WA KUSINI MWA SOMALIA WAKOMBOLEWA NA MAJESHI YA KENYA YAKISHIRIKIANA NA YA SOMALIA.

MJI WA KUDAY WA KUSINI MWA SOMALIA WAKOMBOLEWA NA MAJESHI YA KENYA YAKISHIRIKIANA NA YA SOMALIA.

Written By Unknown on Monday 23 March 2015 | Monday, March 23, 2015

Majeshi ya Kenya yakisaidiana na ya Somalia yamefanikiwa kuukomboa mji wa kiistratijia wa Kuday ulioko kusini mwa Somalia kutoka mikononi  mwa kundi la kigaidi la al Shabab la nchini humo. Kanali David Obonyo Msemaji wa Jeshi la Kenya amesema kuwa, operesheni hiyo ilifanyika kwa mashirikiano kati ya majeshi ya Kenya na yale ya Somalia chini ya usimamizi wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika AMISOM nchini humo. Msemaji wa Jeshi la Kenya amesema kuwa, kwenye operesheni hiyo wanachama kadhaa wa al Shabab wameangamizwa, magari matano yameteketezwa na silaha na zana kadhaa za kivita kuchukuliwa ngawira. Kanali Obonyo ameongeza kuwa, majeshi ya Kenya na Somalia yamefanikiwa kutoa pigo kubwa kwa wanachama wa al Shabab kwenye operesheni hiyo. Kanali Obonyo amebainisha kuwa, mji wa kiistratijia wa Kuday ambao uko kusini mwa bandari ya Kismayu, na ilikuwa ngome muhimu ya kundi la al Shabab. Katika miezi ya hivi karibuni, Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM kimetekeleza operesheni kadhaa zenye lengo la kuwatokomeza wanamgambo wa kundi la al Shabab nchini humo.


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi